KKUTKKUTMfumo wa Kumbukumbu na Taarifa za KKUT

بسم الله الرحمن الرحيم  ·  Bismillahir Rahmaanir Rahiim

KAMATI YA KUENDELEZA UISLAMU TANZANIA (KKUT)

Mfumo wa Kumbukumbu na Taarifa za KKUT

Hifadhi, linda na simamia nyaraka, taarifa na kumbukumbu za Kamati kuanzia ngazi ya Taifa, Kanda, Mkoa, Wilaya hadi Kata.

UsalamaUfuatiliaji
KKUT
10Kanda
8Ngazi za uongozi
7Kamati tanzu
Nyaraka za DijitaliHifadhi salama yenye matoleo
Ripoti za TaasisiWiki, mwezi, robo na mwaka
Miradi na MaliUfuatiliaji wa miradi na mali za KKUT
Matukio na MikutanoVikao, maazimio na tathmini
Usalama
Uwazi
Ufuatiliaji
Usimamizi wa Kumbukumbu

Mtandao wa kitaifa, mfumo mmoja

Kuanzia Taifa hadi Kata: kila ngazi ina dashibodi yake, ruhusa zake na taarifa zake, zote zikiwa salama mahali pamoja.

10Kanda
37Mkoa
8Ngazi za uongozi
7Kamati tanzu

Matukio ya hivi karibuni

Programu ya wahitimu wa vyuo vikuu ikiendelea Chuo Cha Ualimu Cha Kiislamu Kirinjiko

Programu ya wahitimu wa vyuo vikuu ikiendelea Chuo Cha Ualimu Cha Kiislamu Kirinjiko

Vijana wakiwa katika mafunzo ya uongozi na UHUDUMU wa jamii Kirinjiko Islamic Teacher's College

16/10/2026

Programu ya wahitimu wa vyuo vikuu ikiendelea Chuo Cha Ualimu Cha Kiislamu Kirinjiko

Programu ya wahitimu wa vyuo vikuu ikiendelea Chuo Cha Ualimu Cha Kiislamu Kirinjiko

Vijana wakiwa katika mafunzo ya uongozi na UHUDUMU wa jamii Kirinjiko Islamic Teacher's College

16/10/2026

Kuhusu KKUT

Kamati ya Kuendeleza Uislamu Tanzania ni kundi la harakati za kuhuisha na kusimamisha uadilifu katika jamii. Liliasisiwa na wanaharakati kutoka Tanzania Bara na Zanzibar mwezi Desemba 2002, kwa kuzingatia agizo la Allah (s.w) katika Qur'an (3:104).

Kulingania Kheri

Kuhakikisha kila mtu katika jamii anafikishiwa ujumbe sahihi wa Uislamu kinadharia na kivitendo, kupitia programu za watu wa rika zote.

Kuamrisha Mema

Kila mwanakundi awe kigezo cha kufanya mema na kudumu katika kuudhihirisha Uislamu wake kivitendo.

Kukataza Maovu

Kuwa mstari wa mbele katika kuacha maovu kabla ya kuyakataza kwa wengine.

Kamati na malengo yake kwa ufupi

Kamati ya Kuendeleza Uislamu Tanzania (KKUT) ni kundi la harakati za kuhuisha na kusimamisha uadilifu katika jamii, lililoasisiwa na wanaharakati wa Tanzania Bara na Zanzibar mwezi Disemba 2002 kwa mujibu wa Qur'an (3:104).

Mtandao wake unaanzia Taifa, Kanda 10, Mikoa, Wilaya, Majimbo, Kata/Shehia, Mitaa/Vijiji hadi Vitongoji, na tanzu zake ni Walimu, Wanawake, Afya, Ardhi/Ujenzi/Miradi na Uchumi, Madrasa na Waratibu wa Elimu.

Kulingania kheri
Kuamrisha mema
Kukataza maovu
1Safu za uongozi na ofisiMikoa, wilaya na kata zikamilishe safu za uongozi; kila mkoa uwe na ofisi, muhudumu na nyaraka zilizotunzwa.
2DarsaKila wilaya ianzishe na kuimarisha darsa za kata/shehia; kila mkoa uwe na Darsa Duara la wahitimu wa EKP.
3Madrasa kwa MtaalaKuandaa walimu wa AMUU, kuimarisha madrasa za wilaya na kuanzisha madrasa mpya zinazofuata mtaala.
4Elimu ya Kiislamu kwa PostaKusajili wasomaji wapya kila wilaya (viongozi, walimu na watumishi) na kuwafikisha juzuu ya nne.
5Kuandaa walimuSemina za utambuzi, warsha za ufundishaji na kuwashirikisha walimu katika kulea wanafunzi shuleni.
6Elimu ya Dini ya Kiislamu (EDK)EDK ifundishwe shule za msingi na sekondari, wanafunzi wafanye mitihani ya taifa, na takwimu za shule zikamilike.
7Kata/Shehia ProgramuVituo vya masomo ya ziada kwa wanafunzi wa msingi na sekondari kwenye kata.
8Vijana, wanawake, afya na uchumiKambi za wahitimu, programu za wanawake na vijana, huduma za afya, ardhi, miradi, zakat na sadaqat.

Programu za kila sekta

Kamati Kuu ya Kuendeleza Uislamu

Safu za Uongozi (mkoa, wilaya, kata)Ofisi ya mkoa na utunzaji wa kumbukumbuDarsa za Kata/ShehiaDarsa za FamiliaDarsa Duara la wahitimu (EKP/AMUU)Ziara za utendaji za kila mweziKKUT Community Fund

Waratibu wa Elimu na Kamati ya Walimu

Elimu ya Kiislamu kwa Posta (EKP)Ufundishaji wa EDK shuleniMitihani ya Taifa ya EDK/IKUratibu wa Walimu Waislamu (semina, warsha, kulea)Wahitimu wa vyuo vya UalimuKata/Shehia Programu (vituo vya masomo ya ziada)Kambi/Itkaf na semina za wanafunziProgramu ya wahitimu kidato cha nne (kambi)Kuandaa wanafunzi wa vituo vya malezi

Kamati ya Madrasa kwa Mtaala

Madrasa kwa Mtaala

Kamati ya Wanawake Waislamu

Wanawake wanaoshiriki program ngazi ya kataWarsha za wanawakeDarsa za wanawakeMalezi ya watoto (miaka 0-13)

Programu za Vijana (miaka 13-21)

Semina za vijanaDarsa za vijana

Kamati ya Watumishi wa Afya

Takwimu za vituo vya afya na wataalamuElimu ya afya ya msingiKambi za kutolea huduma za afya

Kamati ya Ardhi, Ujenzi, Miradi na Uchumi

Ardhi na urasimishajiUjenzi wa vituoMiradi ya UchumiZakat na Sadaqat (bajeti, mapato na matumizi)

Muundo wa Uongozi

Mtandao wa uongozi unaanzia Taifa, Kanda, Mkoa, Wilaya, Majimbo, Kata/Shehia, Vijiji/Mitaa hadi Kitongoji. Kuna Kanda 10 zinazojumuisha mikoa ya kikamati kama inavyoonekana hapa chini.

Taifa›Kanda›Mkoa›Wilaya›Jimbo›Kata/Shehia›Kijiji/Mtaa›Kitongoji
1Kanda KaskaziniArusha, Kilimanjaro, Tanga
2Kanda KusiniMtwara, Lindi
3Kanda KatiManyara, Dodoma Kaskazini, Singida, Dodoma Kusini
4Kanda Ziwa MasharikiMara, Simiyu, Mwanza
5Kanda Ziwa MagharibiKagera Mashariki, Kagera Magharibi, Shinyanga, Geita
6Kanda MagharibiTabora, Kigoma Mashariki, Kigoma Magharibi, Katavi
7Kanda Nyanda za JuuMbeya, Rukwa, Songwe
8Kanda VisiwaniUnguja, Pemba
9Kanda MasharikiKinondoni, Ubungo, Kigamboni, Ilala, Temeke, Morogoro Kaskazini, Morogoro Kusini, Pwani Kaskazini, Pwani Kusini
10Kanda Nyanda za Juu KusiniRuvuma, Iringa, Njombe

Safu ya viongozi kila ngazi

AmirNaibu AmirKatibuNaibu KatibuMweka HazinaNaibu Mweka HazinaAmiratNaibu AmiratMratibu

Kamati tanzu

Kamati ya Kuendeleza Uislamu

Kamati kuu ya kila ngazi; inasimamia utekelezaji wa majukumu yote ya kamati.

Kamati ya Walimu Waislamu

Walimu Waislamu wa shule za msingi hadi vyuo vikuu, kuanzia mkoa hadi shuleni.

Kamati ya Wanawake Waislamu

Wanawake walio tayari kuutumikia Uislamu na kuleta mabadiliko katika jamii ya wanawake.

Kamati ya Watumishi wa Afya

Wataalamu wa afya Waislamu: kambi za huduma, elimu ya afya na uadilifu kazini.

Ardhi, Ujenzi, Miradi na Uchumi

Ardhi, ujenzi, miradi ya uchumi, bajeti, zaka na sadaka, mapato na matumizi.

Kamati ya Madrasa kwa Mtaala

Kuandaa walimu wa madrasa kupitia kozi ya AMUU na miundombinu ya madrasa za mtaala.

Waratibu wa Elimu

Waratibu wa mkoa, wilaya na kata wanaosimamia Elimu ya Dini ya Kiislamu mashuleni.

Ratiba ya vikao na tathmini

Tamasha la Kitaifa na Semina ya ViongoziMara mbili kwa mwaka (katikati na mwisho wa mwaka)
Mkutano Mkuu wa Mwaka: tathmini ya mwaka mzimaDisemba, Kirinjiko Islamic Centre, Same, Kilimanjaro
Taarifa ya utekelezaji ya kila mkoa (mwaka mzima)Novemba
Vikao vya KandaMara tatu kwa mwaka (cha kwanza kinaongozwa na Taifa)
Shura ya MkoaAprili (masaa 6), Agosti (masaa 6), Disemba (siku nzima)
Mikutano ya mikoaMara moja kwa mwaka, Disemba (masaa 9)
Shura ya Uongozi (Management)Mara moja kila mwezi
Vikao vya UtendajiKila wiki mara moja

Huduma za mfumo

Hifadhi ya Nyaraka (Archive)

Pakia, ainisha, kagua na hifadhi nyaraka kwa matoleo na ruhusa kulingana na ngazi.

Ripoti na Tathmini

Ripoti za wiki, mwezi, robo na mwaka, pamoja na fomu rasmi ya Taarifa ya Mwaka ya Mkoa.

Fedha na Mali

Leja ya mapato na matumizi, stakabadhi, zaka na sadaka, na rejista ya mali za KKUT.

Viongozi na Ngazi

Viongozi, tanzu, mikutano, miradi na maazimio kwa wigo wa Kanda, Mkoa, Wilaya na Kata. Kwa watumiaji walioalikwa pekee.

Ingia

Duka la Vitabu

Nunua vitabu vya Kiislamu mtandaoni bila kujisajili.

Tembelea Duka la Vitabu
Duka la Vitabu

Soma. Jifunze. Hifadhi.

Vitabu vya Kiislamu na vya elimu vilivyochapishwa na Kamati. Nunua kwa dakika chache, bila kujisajili, na usome mara moja kwenye simu au kompyuta.

  • Hakuna usajili
  • Malipo salama ya simu
  • Soma papo hapo au pakua
Vinjari vitabu vyote

Vitabu vipya vinaongezwa hivi karibuni.